Burudani

Bosi wa Kaburu afunguka kuhusu label yake na ishu ya kutoka na Amber Lulu wa Harmorapa (Video)

Bosi wa label ya Kaburu Entertainment, Mr Baburu Entertainment weekend hii katika sherehe yake ya birthday iliyofanyika nyumbani kwake Bunju B jijini Dar es salaam alimtambulisha Amber Lulu kuwa ni mpenzi wake tukio ambalo lilileta taharuki katika mitandao ya kijamii baada ya rapper Harmorapa pia kumtangaza msanii huyo kuwa ni mpenzi wake.

Akiongea na Bongo5 Jumatano hii, Kaburu amedai ishu za Harmorapa kutoka na mrembo yeye hazijui huku akijidai mwenye kisu kikali ndiye atakaye kula nyama.

“Inawezekana nikawa na mahusiano na Amber Lulu au la!, lakini moyo wangu naona kabisa una kitu fulani, namwelewa sana pia ni mshikaji na siyo mtu wa mambo mengi,” alisema Kaburu.”Yeye yuko kwenye entertainment na mimi niko huko kwahiyo kinaweza kutokea kitu chochote siyo tu mahisiano hata kufanya naye kazi,”

Katika hatua nyingine Kaburu amedai studio yake inatoa huduma mbalimbali kwa wasanii wachanga kwa wakubwa katika lengo la kusaidia muziki wa bongofleva kufika mbali zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents