Burudani

Bongo Star Search 2015 yazinduliwa, mengi yaongezeka

Shindano la kuvumbua vipaji vya wanamuziki lililodumu kwa miaka 8 ‘Bongo Star Search’ limezinduliwa tena jijini Dar es salaam huku likija na maboresho mbalimbali chini ya udhamini mkuu kutoka kwa PSI.

IMG_9828
Madam Rita akizungumza na waandishi wa habari Alhamis hii

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamis hii, ndani ya ukumbi wa High Spirit Lounge jijini Dar, Mkurugenzi wa Benchmack Production na mwanzilishi wa shindano hilo, Rita Paulsen alisema mwaka huu wameboresha zaidi shindano hilo.

“Mwaka huu wa 2015 utakuwa ni msimu mzuri na wa kusisimua. Shindano la Bongo Star Search litakuwa kwenye mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza Pia Bongo Star Search itarushwa hewani kupitia na Clouds TV na Star TV. Kwahiyo Mwanza tutakuwa July 4-5 ndani ya ukumbi wa La Kairo, July 11-12 Arusha katika ukumbi wa Triple A Hotel, July 18-19 tutakuwa Mbeya ndani ya ukumbi wa Club Vibes na Dar es Salaam itakuwa tarehe 24-26. Kwahiyo wenye vipaji wakae mkao wa kula,” alisema Madam Rita.

IMG_9829
Madam Rita (kushoto) akiwa na mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo

Pia Madam Rita alisema mshindi kama kawaida atapewa zawadi ambayo bado haijawekwa wazi pamoja na usimamizi kutoka Tip Top Connection.

“Licha ya zawadi kwa mshindi pia Top 5 watakuwa chini ya Tip Top Connection, yaAni Tip Top ndIo itawameneji,”alisema.

“Pia mwaka huu tupo na mbunifu wa mavazi Ally Rehmtullah. Tumegundua kuwa muziki na swagga na mavazi vinaendana kutokana na mambo ya mitandao sasa hivi ili uonekane vizuri inabidi uvae vizuri. Kwahiyo tumegundua tukiunganika na tasnia nzima ya mitindo tutapata wasanii ambao wapo kwenye kiwango cha kimataifa kabisa. Sasa hivi hatuwezi kuimba huku tumevaa vibaya. Sasa hivi ni mwonekano mpya ambayo utaleta mapinduzi katika muziki wetu,” alisema Madam.

IMG_9834
Meneja wa PSI, Gaston Shayo (kushoto) akizungumza na wanahabari

Kwa upande wa mdhamini mkuu wa shindano la Bongo Star Seaach, kupitia meneja wa mauzo wa ISP, Gaston Shayo alisema kupitia kampeni yao ‘Kuwa Original Chagua Original’ ya kuelimisha vijana kutumia kondom, wameona Bongo Star Seach ndicho chombo muafaka cha kuibua vipaji na kuwapa vijana nafasi ya kung’ara pamoja kuwa salama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents