Habari

Bongo Fleva ft. Bongo Movie: Hussein Machozi na Elizabeth Michael ‘Lulu’ katika filamu moja ‘Kafia Ghetto’

Kiwanda cha muziki pamoja na filamu nchini Tanzania vinaendelea kubadilishana ujuzi kati ya wasanii wa muziki na bongo movie, kwani siku za karibuni tumeshuhudia wasanii wengi wa Filamu wakiingia studio na kurekodi nyimbo na wasanii wa muziki kuamua kukaa mbele ya kamera na kujaribu kufanya filamu.

hl

Sasa ni zamu ya msanii wa bongo flevah Hussein Rashid Dodi a.k.a Hussein Machozi kujaribu bahati yake upande wa bongo movie, ambapo anajiandaa kutoa filamu yake mpya inayoitwa ‘Kafia Ghetto’.

Kwa usiyefahamu ‘Kafia ghetto’ ni moja kati ya nyimbo za mwanzo kabisa za Hussein Machozi aliyoirekodi Mwanza katika studio ya Tetemesha Records, ambao ulifanya vizuri zaidi mikoani miaka kadhaa iliyopita wakati Hussein anaanza kujulikana.

Ikiwa ndio movie yake ya kwanza toka aanze kufanya muziki, Machozi amesema ili kuiongezea utamu movie hiyo ameamua kuigiza na staa wa bongo movie Elizabeth Michael a.k.a Lulu ambaye ndiye msichana atakayefia Ghetto katika filamu hiyo.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania Staa huyo wa ‘Kwaajili yako’, ameongeza kwa kumtaja msanii mwingine nguli wa bongo movie Charles Magali maarufu kama Mzee Magali kuwa ni miongoni mwa waigizaji waliohusika katika movie hiyo.

Kama hujawahi kuusikia wimbo wa Kafia Ghetto, story iliyobeba wimbo huo ni ya Hussein na msichana aliyetokea kumpenda lakini hakuwa tayari kumkubalia Machozi waingie kwenye mapenzi, lakini siku moja msichana huyo aliamua kumsuprise Hussein kwa kwenda kumtembelea ghetto kwake na katika ugeni huo binti alimkubalia rasmi Hussein awe mpenzi wake.

Story inaendelea kwa Hussein akiwa mwenye furaha aliondoka chumbani kwenda dukani kununua vinywaji akiwa na furaha, aliporudi ndani ghafla alikuta binti kajilaza kitandani na haongei , ndipo akagundua kuwa amekata roho. So kasheshe ndio ikawa hapo binti wa watu amefia ghetto kwa Hussein na hajui atamtoaje wala itakuwaje majirani wakijua. Hiyo ndiyo story ya wimbo wenywe ambayo naamini katika movie itakuwa imeboreshwa zaidi.

Machozi amesema filamu hiyo imeshakamilika na inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Tazama video ya wimbo wa Kafia ghetto

http://youtu.be/sMd7sgNNF8s

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents