Burudani

Trevor Noah ajitoa kusherehesha tuzo za MTV MAMA, Bonang Matheba achukua nafasi yake

Mtangazaji na mchumba wa rapper wa Afrika Kusini, AKA, Bonang Matheba ametangazwa kuwa mshereheshaji wa tuzo za mwaka huu za MTV MAMA akichukua nafasi ya mchekeshaji Trevor Noah aliyetangaza kutoshiriki.

14676805_1687107708272240_8529433097098231808_n

Trevor ametangaza kujitoa kwenye nafasi hiyo ya kusherehesha kwenye tuzo hizo kama ilivyotangazwa mwanzo sababu ikiwa ni kuumwa hivyo dokta wake akimtaka apumzike hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa aliyoiweka kwenye mtandao wake wa Twitter.

noah

Baada ya kutangazwa kuchukua nafasi ya Noah, Matheba kupitia mtandao wa Instagram ameandika, “UNREAL!!! Just so freakin’ UNREAL!! I feel like I’m being pranked… the BIGGEST MOMENT OF MY LIFE and I only have 24 hours to prepare!! Thank you @mtvbaseafrica for trusting me with this… such a HUGE responsibility… WOW!! ???????????????????????????????????????????? Africa, see you tomorrow night!.”

14719080_1599712623667039_2762181046735732736_n

Tuzo hizo zitafanyika Oktoba 22, 2016, kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome, Johannesburg, Afrika Kusini. Future, Yemi Alade, Ycee, Alikiba, Cassper Nyovest, Diamond, Babes Wodumo, Nasty C, Patoranking, Kwesta na Emtee wanatarajiwa kuwasha moto kwa kutumbuiza kwenye tuzo hizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents