Habari

Boko Haram wamteka mke wa makamu waziri mkuu wa Cameroon

Wanamgambo wa kundi la Boko Haram, wamemteka mke wa makamu wa waziri mkuu wa Cameron, na kuwaua watu watatu baada ya kuushambulia mji wa kaskazini wa Kolofata.

Coleman_BeatingBokoHaram

Wanamgambo hao walivamia makazi ya waziri Amadou Ali huko Kolofata na kumteka mke wake. Kiongozi wa dini ambaye pia ni meya wa mji huo Seini Boukar Lamine naye alitekwa katika shambulio tofauti.

Boko Haram, kundi la wanamgambo wa kiislamu la Nigeria limeingia Cameroon hivi karibuni baada ya nchi hiyo kutuma wanajeshi kuungana na majeshi ya kimataifa kupambana na wanamgambo hao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents