Burudani

Bob Junior kutoa wimbo aliomshirikisha Shaa, collabo na Chameleone yasubiri

Msanii na mtayarishaji wa muziki wa Sharobaro Records, Bob Junior amesema ile ngoma waliofanya na Jose Chameleone haitatoka mapema kama alivyokuwa amepanga na badala yake atatoa ngoma nyingine kama bonus huku akiweka mambo sawa kwaajili ya collabo hiyo.

bob-n-jose

Kutokana na kubadilika kwa mipango hiyo, msanii huyo amesema atatoa wimbo aliomshirikisha Shaa.

“Unajua Jose amekuwa yupo busy sana na huwezi kumuingilia mtu wakati ukute tayari ana mikataba ya hizo show,” amesema Bob.

“Samahani tu kwa mashabiki zangu ila kuna ngoma nitatoa mwezi huu wa Ramadhan, nimefanya na Shaa ni ngoma ya kudance inaitwa ‘Bado Bado’, nitatoa video pamoja na audio kwa pamoja. Unajua mimi nina album kwahiyo na ngoma nyingi hiyo ndio nimeona niitoe kwa sasa, ila ile ngoma na Jose ipo pale pale.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents