Burudani

Bob Junior kufanya show ya ‘Usiku wa Masharobaro’ kutimiza miaka 8, atatoa tuzo kwa waliomsaidia

Msanii wa muziki na producer wa Sharobaro Records, Bob Junior amedai anatarajia kufanya show ya usiku wa masharobaro ambapo amedai atatoa tuzo kwa wadau waliomsaidia kufika hapo alipo.

sharo bob junior

Bob Junior ameiambia Bongo5 kuwa show hiyo itakayofanyika August 3 mwaka huu itahudhuriwa na wasanii wote waliowahi kufanya ngoma Sharobaro Records.

“Natarajia kufanya show ya usiku wa Masharobaro ndani ya Maisha Club tarehe 3 mwezi wa nane mwaka huu yaani ni show ya kwanza Jumapili Maisha Club tunafungua sisi,” amesema. “Wasanii wote ambao wamefanya hits kutoka Sharobaro records nitawaalika. Wasanii ambao watanisupport bado sijawapanga. Bob Junior nitafanya show ya kitofauti kabisa na nitatoa certificate au tuzo kwa media zote na namaanisha kuanzia blogs, TV station na redio na magazine. Kwahiyo kutakuwa na vitu vikubwa sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents