Burudani

Bob Junior atoa sababu ya nyimbo zake za sasa kushindwa kufika mbali

Msanii wa muziki na producer wa Sharobaro Records, Bob Junior amefunguka na kutoa sababu ya kwanini nyimbo zake nyingi za sasa kutokuwa na uhai mrefu kama za mwanzo.

sharo bob junior
Bob Junior

Bob Junior aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Oyoyo’ ameiambia Bongo5 kuwa, muziki wake kwa sasa hivi unaharibiwa na mitandao ya kijamii.

“Nyimbo nyingi hazi-play sana kwenye radio, zinachukua nafasi kubwa kwenye social network kwa upande wangu, lakini ukiangalia ni nyimbo nyingi hazikai, siyo kama zamani na siyo kwangu mimi tu hata kwa wasanii wengine, kwaiyo muziki umebadilika, tatizo mimi nadhani ni social media kwa sababu zinapata nyimbo za watu mapema kwenye simu zao, pia social network zamani ndiyo ilikuwa imeanza kuharibu mfumo wa albam, mtu anapata wimbo mapema na anausikiliza zaidi ya mara kumi halafu anaichoka,” alisema Bob Junior

Katika hatua nyingine Bob Junior amezungumzia kukamilika kwa kazi yake aliyomshirikisha Jose Chameleon ambayo itatoka ndani ya mwaka huu.

“Nina wimbo na Chameleon ambao umeshaisha na nitaanza ku-promote kuanzia jumamosi, kwahiyo inaweza ikatangulia audio halafu ikaja video kabisa,” alimaliza Bob Junior.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents