Habari

Blogger mtata wa Kenya ashtakiwa kwa kumuita Kenyatta ‘Rais Mtoto’

Blogger maarufu wa Kenya mwenye ushawishi mkubwa kwenye Twitter, Robert Alai ameshtakiwa kwa kumdhihaki Rais Uhuru Kenyatta kwa tweet aliyoandika mapema wiki hii.

_79793845_alai624

Alai ambaye ni mkosoaji mkubwa wa serikali, alimuita Kenyatta ‘Rais Mtoto’.

Amekanusha madai hayo na alitolewa kwa dhamana ya $2,000 na kuonywa kutoandika tweets za aina hiyo wakati uchunguzi ukiendelea.

Alai ana followers zaidi ya 141,000 kwenye Twitter. Siku hiyo hiyo alipoandika tweet hiyo, alipost pia namba ya Kenyatta na za maafisa wengine wa juu.

Wakenya wengi wanaoamini mashtaka hayo ni sehemu ya mpango wa serikali kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na wa kujieleza, wamemuunga mkono kwa Alai.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents