Burudani

Black Rhino aeleza faida za msanii kurekodi nyimbo nyingi na kuziweka maktaba

Rapper Black Rhino anawakumbusha wasanii wenzake faida za kurekodi nyimbo nyingi kila wanapopata muda na kuzihifadhi maktaba kwaajili ya matumizi ya baadae hata watakapoaga dunia.

Black

Rhino amesema faida ya kwanza msanii anapokuwa na akiba kubwa ya nyimbo ni hata atakapoaga dunia, nyimbo zake mpya zitaendelea kubaki na kuwafaidisha ndugu kutokana na mauzo ya albums.

“Ni jambo zuri kwa msanii kurekodi ngoma zako tu kwa muda wako mwingi wa kutosha hata kama ukiwa unarekodi ngoma zingine for future, ni vizuri sana kutengeneza kama library ya muziki wako, Kuna lolote linaweza likatokea.” Alisema Black Rhyno kupitia Planet Bongo ya EA Radio.

Rapper huyo ametoa mfano wa Tupac Shakur ambaye hata baada ya kufariki nyimbo zake mpya ziliendelea kutoka na kuwafaidisha ndugu zake pamoja na mashabiki.

“Hata kwa wenzetu tunaweza kuona kwa mfano marehemu Tupac alikuwa anarekodi ngoma nyingi sana anaziweka library, Tupac alifariki lakini ngoma zake zilibaki library nyingi sana ambazo sasa zikaendelea kuuzwa na familia yake ikaendelea kufaidika kutokana na kazi yake ya sanaa aliyokuwa akiifanya.”

Faida nyingine aliyoitaja Black Rhyno ni pale msanii anapojikuta yuko busy hawezi kuingia studio kurekodi nyimbo mpya, ndio ambapo anaweza kuchagua wimbo wa kutoa kutoka katika zile alizoziweka maktaba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents