Habari

Binti wa Desmond Tutu afutwa kazi ya ukasisi baada ya kufunga ndoa ya jinsia moja

Mtoto wa askofu mstaafu wa kanisa la kianglikana nchini Afrika Kusini, Desmond Tutu amefutwa kazi yake ya ukasisi wa kanisani baada ya kufunga ndoa na mwanamke mwenzake.

IMG_9360

Mpho Tutu aliyekuwa akihudumia kwenye kanisa la Anglikana alifunga ndoa hiyo mwezi uliopita na Prof Marceline van Furth huku sheria za nchi hiyo zikiruhusu ndoa hiyo ya jinsia moja kutokana na sheria iliyopitishwa Novemba 30, 2006. Lakini kanisa hilo la Anglikana la Afrika Kusini bado limeendelea kupinga ndoa hizo za jinsia moja.

Aidha baada ya kitendo hicho alichokifanya Mpho Tutu kanisa la Anglikana la Afrika Kusini limeamua kumvua madaraka yote aliyokuwa nayo kwenye kanisa hilo kama kuongoza ibada ibada takatifu za kanisa hilo pamoja na shughuli zote za kikanisa.

Hata hivyo Bi Tutu amekiri kuwa sheria za kanisa hilo la kianglikana nchini Afrika kusini zinaeleza wazi kuwa ndoa iliyoruhusiwa ni kati ya mwanamke na mwanaume pekee. Baada ya kufunga ndoa hiyo askofu wa kanisa la Saldanha Bay alishauriwa kufuta leseni yake, lakini Bi Tutu aliamua kuirejesha yeye mwenyewe kabla ya kunyang’anywa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents