Michezo

Bingwa wa mbio za wanawake Mariya Savinova akutana na rungu la CAS

By  | 

Mshindi wa mbio za mita 800 za mjini London mwaka 2012, Mariya Savinova kutoka Urusi amevuliwa taji hilo na kupigwa marufuku kutokana na kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli zilizokatazwa michezoni.

Kutokana na taarifa iliyotolewa na mahakama inayosikiliza makosa ya kimichezo (CAS) imesema, Mariya amekuwa akitumia dawa hizo toka mwaka 2010 mpaka 2013 aliposimamishwa kwa uchunguzi zaidi.

“On the basis of clear evidence, including the evidence derived from her biological passport, Mariya Savinova-Farnosova is found to have been engaged in using doping from 26 July 2010 through to 19 August 2013,”: imesema taarifa ya mahakama hiyo.

Pia mwanariadha huyo atapoteza medali yake ya dhahabu aliyoshinda katika mbio za mita 800 za mwaka 2011 katika mashindano ya mataifa bingwa barani Ulaya, pamoja na medali nyingine alizowahi kushinda mwaka 2010 na 2013.

Mariya Savinova amefungiwa kutojihusisha na mchezo huo hadi mwaka 2019.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments