Burudani

Billnass amvuta Country Boy LFLG

Msanii wa muziki wa hip hop, Country Boy ameamua kujiunga rasmi na Petit Man chini ya meneja Mchafu kwa mwaka 2017, ili kuweza kutangaza muziki wake Kimataifa zaidi.

Rapper huyo alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV kuwa ameamua kujiunga na ‘lebo’ ya Live First Live Good ‘LFLG’ kwa mwaka huu kwa kuwa ni menejiment iliyokuwa ikimsapot chini kwa chini tangu zamani huku wakimpa ‘chance’ ya kumchunguza kwa upande wa nidhamu na amesema anajisikia furaha kujiunga na lebo hiyo.

Hata hivyo Country Boy amesema hiyo ni lebo ambayo imeweza kumtoa msanii Bill Nass kupitia ngoma ya Chafu Pozi na muziki wake kufanya vizuri hivyo anaamini yupo kwenye mikono salama na muziki wake utafika mbali zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents