Burudani

Bill Nas: Watu walinishauri nisiachie ‘Mazoea’ kwa kuwa ulikuwa ni wimbo wangu wa pili

Bill Nas amefunguka sababu ya kuchelewa kuachia wimbo wake wa ‘Mazoea’ ambao amemshirikisha Mwana FA.

Raper huyo amewahi kusema kuwa wimbo huo ulitakiwa uwe wimbo wake wa pili baada ya ule wa ‘Raha’ kwa kuwa alikuwa ameshaurekodi tangu mwaka 2014 kilichokuwa kikisubiriwa ni verse ya Mwana FA pekee.

“Kihalali baada ya ‘Raha’ hii ilitakiwa iwe nyimbo yangu ya pili. Watu walikuwa wananiambia wimbo wako wa pili tu unasema hutaki mazoea inakuwa haileti picha nzuri, lakini imekuwa mpya zaidi baada ya kuona verse ya Mwana FA,” Bill Nas amekiambia kipindi cha Artist of the Day cha Dizzim Online.

“Mimi mwenyewe nimeipenda zaidi baada ya kuiona verse ya Mwana FA na test pia imebadilika na pia nashukuru Mr T yupo mbele ya muda kwa sababu hiyo beat amepiga kipindi hicho lakini ukiisikia sasa hivi ni ya kisasa zaidi,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents