Burudani

Bill Nas adai mfumo wa muziki unawakwamisha wasanii wa Hip Hop

Mkali wa ‘Ligi ndogo’ Bill Nas amesema wasanii wengi wa Hip Hop wanashindwa kufanya vizuri kutokana na mfumo wa muziki nchini kuwapa nafasi zaidi wasanii wa muziki wa kuimba.
Bill Nas

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Bill Nas alisema hali hiyo imewafanya wasanii wa Hip Hop wazidiwe nguvu na wale wa kuimba.

“Tatizo kubwa ambalo mimi naliona ni mfumo tu wa muziki wetu. Kwa sababu ukimzungumzia mtu kama County Boy, Young Killer, Stamina mimi naamini wote wana uwezo mkubwa, lakini muziki ulivyo ndiyo unafanya waonekana wakawaida,” alisema Bill Nas

Aliongeza, “Kiukweli hata mimi naona muziki wa Hip Hop haufanyi vizuri kabisa. Tumeona wasanii wa Hip Hop sasa hivi wanafanya nyimbo kali, video kali lakini tunazidiwa kwenye nguvu. Mimi naamini nguvu imebadilika, zamani ulikuwa ukimzungumzia Professor Jay hakuna msanii wowote wa kuimba unaweza kumlinganisha nae kwa ukubwa. Kwahiyo kwetu sisi nikinyume, waimbaji wamekuwa na nguvu kubwa kuliko watu wa Hip Hop, na hii imetokana na wasikilizaji wanapewa sana muziki wa kuimba kuliko Hip Hop.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents