Burudani

Beyonce kutumbuiza kwenye tuzo za Grammy mwaka huu

Beyonce na Jay Z kwa sasa wameteka vichwa vya habari baada ya kutangaza ujio watoto wao wengine mapacha. Waandaaji wa tuzo za Grammy ambazo kwa mwaka huu zitakuwa za 59 kufanyika tangu zilipoanzishwa wamemtangaza Queen Bey kuwa miongoni mwa wasanii wanaotarajiwa kutumbuiza tuzo hizo mwaka huu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Entertainment Tonight umedai kuwa Queen Bey kwa sasa anafanya mazoezi ya kujiandaa na show hiyo kwa siri mjini Los Angeles.

Wasanii wengine wanaotarajiwa kutumbuiza kwenye tuzo hizo ni pamoja na Adele, John Legend, Bruno Mars, The Weeknd, Alicia Keys, Chance the Rapper, A Tribe Called Quest, Anderson Paak na wengine.

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Jumapili ya February 12, 2017 katika ukumbi wa Staples Center uliopo mjini Los Angeles huku mchekeshaji maarufu James Corden.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents