Burudani

Beyonce ajitoa kutumbuiza kwenye Coachella, mauzo ya tiketi yashuka kwa asilimia 12

Beyonce, amelazimika kusitisha kwenda kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella Valley Music and Arts, mwaka huu.

Tangazo hilo limekuja miezi miwili kabla ya tamasha hilo kufanyika, April 15-17. Bey ameamua kuahirisha kutokana na kuwa mjamzito.

Muimbaji huyo mwenye ujauzito wa watoto mapacha, amelazimika kujiondoa kutokana na ushauri wa madaktari. Tangazo hilo limesababisha kushuka kwa mauzo ya tiketi kwa asilimia 12.

Coachella ndio tamasha linaloingiza fedha nyingi zaidi duniani. Mwaka jana liliingiza dola milioni 94.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents