Burudani

Jay Z na Beyonce kuingiza dola milioni 82 kwenye ziara ya ‘On The Run’

Ndoa yao inaweza kuwa kwenye mawe kama tetesi zinavyosema lakini Jay Z na Beyonce wana kitu cha kujiliwaza kwakuwa wataingiza mkwanja wa kutosha On The Run tour.

cigars-and-laughter-beyonce-jay-z-6th-anniversary-vacation-dominican-republic-the-jasmine-brand

Vyanzo vimesema kuwa Jay, 44, na mke wake Bey, 32, wataingiza zaidi ya dola milioni 82 wakati mauzo yatafikia dola milioni 101.

Hata hivyo pamoja na neema hizo, kuna kila dalili kuwa Beyoncé yupo mguu nje ndani kwakuwa anadaiwa kwenda kusaka nyumba ya kununua bila kumshrikisha Jay Z, vyanzo vililiambia gazeti la New York Post.

Mrembo huyo alienda kuangalia nyumba yenye thamani ya dola milioni 21.5 huko Chelsea mapema mwezi uliopita – wiki chache baada ya video inayoonesha mdogo wake Solange Knowles akigombana na Jay kwenye lifti.

“Alikuwa mkimya sana kama vile alikuwa anajificha,” kilisema chanzo. Chanzo hicho kimesema mara zote Jay Z huhusika kwa kiasi kikubwa katika utafutaji wa nyumba na hivyo huenda Beyoncé anatafuta nyumba yake mwenyewe atakayoishi na mwanae Blue Ivy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents