Habari

Besta yuko Hot Hot Hot.. lakini bikira!

BestaAina ya muziki, mavazi na muonekano ambao amekuwa akitokea nao katika video zake ndivyo vitu ambavyo vimemfanya msichana Besta kujipatia sifa katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

BestaAina ya muziki, mavazi na muonekano ambao amekuwa akitokea nao katika video zake ndivyo vitu ambavyo vimemfanya msichana Besta kujipatia sifa katika medani ya muziki wa kizazi kipya.

 

Ana macho mazuri, lips nene zenye kumfanya avutie, shepu na rangi ya ngozi yake ni ya kibantu halisi, kiuno cha nyigu kilichoyafanya makalio yakae katika mpangilio wake.

 

Jina lake kamili ni Besta Prosper mtoto wa kihaya aliyemaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya msalato iliyopo mkoani morogoro na baada ya hapo St. Mary’s ambapo alimaliza kidato cha sita na hivi sasa amehitimu Nkumba University nchini Uganda ambapo amechukua shahada ya Business and Information Technology (IT), unaweza kumweka msanii huyu katika list ya wasanii wasomi hapa nchini.

 

Hivi karibuni alipata mchongo wa kupiga show tatu kwenye tamasha kubwa huko nchini Brazil, lililoandaliwa na kampuni moja ya kutengeneza mavazi maalum kwa ajili ya uzinduzi wa aina mpya ya viwalo.

 

“Mimi ni msanii wa kwanza kutoka East Africa kuchaguliwa kushiriki katika tamasha hilo, prodyuza wangu ndiye aliyenipa hiyo connection baada ya yeye kuipeleka video yangu huko na kwa bahati nzuri nikachaguliwa.”

 

Katika video za msanii huyu amekuwa akipendelea kuonesha mwili wake na juu ya hiliamedai kuwa anazimia kutoka na mapigo ambayo yanaendana na aina ya wimbo, eneo na pia anazingatia muongozo (script), havai tu ilimradi ameonekana kwenye video. “Si kama napenda mavazi ya uchi, najali sana kupendeza zaidi. Siwezi kukubali kutokea kwenye video vibaya, najiamini niko hot, sexy na navutia!”

 

“Sina, sijawahi kuwa na mwanaume na wala sitafuti” alisema Besta huku akipepesa macho kama asiye na uhakika na anachosema alipoulizwa kama ana mpenzi.

 

Alikana kabisa juu ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote, jambo ambalo lilipelekea kutupa hisia za kuwa huenda binti huyu ni bikra na alipoulizwa kuhusu hilo pia alikuwa mgumu kutoa ushirikiano kwa madai kuwa hapendi kuweka mezani mambo yake ya ndani.

 

“Mara nyingine huwa inatokea navutiwa na mtu lakini sipati kabisa hisia za kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi kwani naona time yangu bado.”

 

Besta haamini kama kuna msanii anayeweza kuwa zaidi yake hapa nchini, isipokuwa wapo anaowakubali akiwemo Enika upande wa R n’B na Ray C upande wa video, na kwa wasanii wa kiume anakoma na MB Dogg, Joh Makini na Fid Q. “Sifanyi muziki kwa kuangalia nani nimfunike, ninachofanya ni kujitahidi kubuni kitu kizuri na bora ili sanaa yangu isonge mbele” alisema.

 

Bofya hapa kuangalia video za Besta “Kama Ulivyo” na “Baby Boy”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents