Michezo

Benni McCarthy: Mourinho akiwa Man Utd ndiye ataweza kumkabili Guardiola

Mshambuliaji wa zamani wa South Afrika na Klabu ya Porto, Benni McCarthy anasema Jose Mourinho ndiye afaaye zaidi kusaidia Manchester United kukabiliana vilivyo na Manchester City watakaokuwa chini ya Pep Guardiola msimu ujao.

JS60948280

BBC imefahamu kwamba huenda Mourinho, 53, aliyekuwa meneja wa Chelsea, huenda akateuliwa kumrithi Louis van Gaal kama meneja Old Trafford majira yajayo ya joto.
McCarthy, 38, alicheza chini ya Mourinho raia huyo wa Ureno alipokuwa kocha wa Porto.
“Mourinho ni mmoja wa watu wanaojua jinsi ya kumshinda Guardiola na mbinu zake,” ameambia BBC Sport.

“Alipokuwa Real Madrid, alimshinda mara kadha. AKiwa Inter Milan, alifanikiwa pia dhidi yake (Guardiola).

“Kwa sasa sioni mtu yeyote anayeweza kumkabili Pep na mbinu zake Manchester City isipokuwa tu Mourinho akiwa United, atakwua na rasilimali, wachezaji na usaidizi wa kifedha wa kukabiliana na Guardiola.”
Guardiola, alikuwa kocha wa Barcelona, kwa sasa ni mkufunzi mkuu wa Bayern Munich.
Klabu ya Manchester City ilitangaza majuzi kwamba atamrithi Manuel Pellegrini majira yajayo ya joto.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents