Burudani

Ben Pol na Bi Kiroboto waigiza kama mama na mwanaye katika filamu ya ‘Sunshine’ inayotarajiwa kutoka wiki ijayo

Mwimbaji wa R n B Ben Pol ambaye wiki hii ameachia single mpya ‘Unanichora’ pamoja na album mpya, wiki ijayo upande wa pili wa kipaji chake utaonekana katika filamu mpya aliyoigiza pamoja na mchekeshaji wa kike Bi Kiroboto inayoitwa ‘Sunshine’.

SUNSHINE movie

Katika filamu hiyo iliyotayarishwa na Swahiliwood Production, Ben Pol na Christina Mbunda maarufu kama bi Kiroboto wameigiza kama mama na mwanaye.

Akizungumza na Tovuti ya TIMES FM mratibu wa Swahiliwood Hassan Mrope, amesema kuwa filamu hiyo itazinduliwa February 20 kuanzia saa kumi na mbili jioni katika jumba la sinema Century Cinemax, iliyoko Oysterbay, Dar es Salaam.

Mrope amesema filamu hiyo itazinduliwa pamoja na filamu zingine mbili ambazo ni ‘Network’ na ‘Mdundiko’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents