Burudani

Ben Pol azungumzia wimbo mpya ‘Twaendana’ atakaoutoa wiki ijayo, ni wimbo wa ubia na producer

Mwimbaji wa R&B Tanzania, Ben Pol Jumatatu ijayo (August 25) anatarajia kuachia wimbo mpya wa R&B ambao utakuwa ni wa ubia na producer wa Noiz maker.

Noiz na Ben Pol

Ben Pol ameiambia Bongo 5 kuwa ameingia ubia na DX wa Arusha ambao wamegawana haki za wimbo huo.

Ben Pol akiwa napiga Piano

“nimeimba wimbo wote lakini nadhani ni wimbo wa kwanza kuwa na partnership na producer”, Alisema Ben Pol. “Kwa huu wimbo mimi na bwana DX kila mtu ana haki nyingi nyingi, japo tutashare gharama za video na promotion pia lakini yeye atasimamia upande wa mauzo ya online.”

Ben Pol ameongeza kuwa ni kawaida yake kutoa wimbo wa R&B kila mwisho wa mwaka, hivyo ‘Twaendana’ ambao ni wimbo wa R&B, ndio official single baada ya ‘Upendo’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents