Burudani

Ben Pol adai Sophia inampa neema nyingi

Ben Pol amesema wimbo wake Sophia umemfanya apate mashabiki wengi wapya ambapo wengine wanadhani wimbo huo ndo wimbo wake wa kwanza.

Ben Pol

Akizungumza na Bongo5 jana, Ben Pol alisema wimbo huo umemfanya apate bookings nyingi kuliko zingine.

“Sophia kwanza imenipeleka mahali ambako sikuwepo,” amesema. “Imeniongezea mashabiki wapya wengi sana ambao hata walikuwa hawanijui kabisa, tena wanajua ndio wimbo wangu wa kwanza.

Kwa mafanikio ya kwanza ya huu wimbo umeniletea mashabiki wapya. Pili huu wimbo nimekuwa booked sana kila kona napigiwa simu kwenda kufanya show. Hii ni ishara nzuri kwamba wimbo umeeleweka na pia umeingiza pesa nzuri,” aliongeza Ben Pol.

Ben Pol amesema anajipanga kuachia kazi mpya hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents