Burudani

Ben Pol adai mapokezi ya Sophia yamemtisha kiasi cha kuifumua idea ya mwanzo ya video

Ben Pol amedai kuwa mapokezi ya wimbo wake mpya Sophia yamekuwa makubwa kuzidi matarajio yake kiasi kwamba amelazimika kurudi kwenye ‘drawing board’ kupanga upya jinsi atakavyotakiwa kuifanya video yake.

10932191_1545721332379090_380810471_n

Amedai kuwa awali alikuwa amepanga kuanza na video ya wimbo huo, mpango ambao uliahirishwa kwa mara mbili.

“Lakini plan yetu tulivyokuwa tumeitengeneza kiasi kwamba huwezi amini sasa hivi tumeamua kufumua ule mpango wa video tuliokuwa nao mwanzo na kuweka maboresho labda mara zaidi ya mwanzo. Wimbo umekuwa mkubwa na watu wanaonekana hawatarajii disappointment yoyote kwenye video,” amesema Ben Pol.

“Imebidi tukae tena mezani tuweze kutafuta namna ya kuutunisha mfuko wa bajeti ya video yake.”

Ben amesema asingependa kuchelewesha video ya wimbo huo hivyo mipango yake ni kuhakikisha inatoka mwezi ujao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents