Burudani

Ben Pol adai alikuwa haamini kama atafanikiwa bila kuwa na management

Mwimbaji wa R&B, Ben Pol amesema alikuwa haamini kama ataweza kutoka kimuziki bila kuwa na managament ya kumsimamia.

Bon-Pol-II

“Mimi nilivyotoka kwenye lebo mwaka 2011, nilikuwa sina confidence ya kusema kwamba nitaweza kufanya muziki mwenyewe, sina record label. Lakini marafiki zangu wachache waliokuwa wanasikiliza nyimbo zangu na wengine ambao walikuwa kwenye media, walikuwa wanatumia nguvu yao kubwa sana kuwahamasisha watu kwamba huu muziki ni mzuri. Na kupitia nguvu yao ikabadilisha ikawa kitu kikubwa nchi nzima mpaka na sehemu za karibu zote watu wakawa wanasapoti,” Ben Pol ameiambia Planet Bongo ya EA Radio.

Aliongeza, “mpaka mwaka 2012 nashinda tuzo ya wimbo bora wa R&B niko nyumbani naangalia tuzo kwenye TV. Kwa sababu najua naweza nisipate kwa sababu sina record label.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents