Burudani

Belle 9: Kwanini wabongo hatutaki kukubali Diamond ni msanii mkubwa Afrika?

Belle 9 amekana kusaini na WCB na kudai kuwa alienda kutembelea kwenye ofisi zao kwakuwa Diamond ni msanii mkubwa Afrika na amefanikiwa kufika mbali kimuziki.

Daimond-na-Belle-9

“Diamond ni msanii mkubwa Afrika ila Watanzania tumekuwa wagumu kulikubali hilo,” amekiambia kipindi cha E News cha EATV. Belle 9 aliongeza kuwa alienda WCB kwa ajili ya kuwatembelea na kufanya nao mazoezi kwa sababu anamheshimu Babutale kwakuwa ndiye aliyemkutanisha na menejimenti yake aliyonayo.

Katika hatua nyingine, muimbaji huyo amesema kuwa bado ana mkataba na menejimenti yake hivyo hawezi kusaini mkataba kwingine labda mpaka utakapomalizika. Na kuhusu WCB amesema anaweza akasaini nao endapo wakikubaliana na mambo yakienda sawa.

Hata kwa Rich Mavoko ilikuwa ni sinemaa kama hii lakini hatimaye alijiunga na familia ya Wasafi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents