Burudani

Belle 9 auzungumzia wimbo wake mpya Vitamin Music

Belle 9 ameachia wimbo wake mpya ‘Vitamin Music’ aliomshirikisha Joh Makini.

10632890_344928349018708_6701426134620419848_n

Akizungumza na XXL ya Clouds FM jana, Belle alisema wimbo huo ni sehemu ya project yake mpya ya album yenye jina hilo.

“Ngoma tulifanya kwa Mona Gangster, Classic Sounds lakini mimi sikumtafuta Joh na yeye hakunitafuta, ni ushikaji tu wa muda mrefu, akija studio anasikiliza kazi zangu. Mimi naona siku hizi idea nyingi ambazo nimeshazifanya naona nina wito wa kufanya Vitamin, kwa sababu kila siku napenda kufanya kitu tofauti. Kwahiyo naona kama huu ni muda wake kutoka wa hii track japo ni ya muda mrefu. Project Vitamin muziki ni album yangu mimi ya pili ambayo tayari ipo studio lakini kwenye Vitamin Music wimbo wenyewe ndio huu ulikuwa unabeba album. Kwahiyo nilipata idea baadaye nikaifanyia kazi, bro akasikiliza na yeye pia akafanya kazi kwenye verse ikawa track. Nimetoa hivi nikiangalia nina track nyingi halafu track ambazo ninazo hii ni tofauti sana na zile,” alisema.

Katika hatua nyingine Belle alizungumzia pia wimbo aliofanya nchini Ujerumani.

“Ile ilikuwa project ambayo nishaanza kuitengeneza lakini sasa hivi siwezi kiongelea haijakamilika. Mimi nilienda kuwakilisha kwa sababu mimi ni mmoja kati ya watu ambao wanashare hiyo idea kwaajili ya project ambayo itakuja bongo na kurudi tena Ujerumani, sasa katika movement zangu nikajikuta niko pale Universal Studio, nikaenda studio nikafanya kazi, video mna vitu kibao,” alisema Belle.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents