Burudani

Belle 9 asema Suma Lee na Queen Darleen ndio waliogundua kipaji chake

Msanii wa Morogoro, Belle 9 amesema Suma Lee na Queen Darleen ndio waliogundua kipaji chake kipindi wasanii hao walipoenda mkoani Morogoro kwenye show wakati huo akiwa bado underground.

Belle

Belle amesema alifanya show kabla ya wasanii hao kupanda na ndipo Suma Lee alipomwambia promota aitwaye Bonga kuwa ‘dogo anaweza mchukue’. Baada ya hapo anasema ‘nilienda kupiga picha na Suma Lee na Queen Darleen, hiyo picha hadi leo ninayo. Nakumbuka wali inunulia na soda wakaniambia ‘dogo unaweza sana’ ndipo baadaye nikachukua namba za Bonga ndo nikaja Dar nikarekodi kwenye studio za G Records producer alikuwa KGT,” Belle 9 ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Nakumbuka nilirekodi chorus tu, nilikaa tu Dar baadaye nikwambia Bonga kwakuwa yeye ndo alinileta Dar, nikamwambia ‘ngoja mie nirudi tu home Moro’ hapo akanimbia ‘sawa basi hamna shida nitafanya mpango basi uipate ile beat’. Akanimbia atafanya mpango nipate ile beat niandikie. Hizo ndo moja ya husstle nilizopitia kabla sijatoka. Huwa wananikumbuka hadi leo nawasiliana nao.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents