Burudani

Bella adai ni hatua mbaya kwa Diamond na Ommy Dimpoz kutupiana maneno machafu mtandaoni (Video)

Mkali wa masauti Christian Bella amedai yeye ni mmoja kati ya watu ambao hawakupenda kuona Diamond na Ommy Dimpoz wakigombana mitandaoni mpaka kufikia hatua ya kurushiana maneno ya kashfa.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nisheke’ ameiambia Bongo5 kuwa hatua ya wasanii kutukanana mitandaoni inaleta picha mbaya kwa mashabiki.

“Kushindana sio kitu kibaya kunamfanya msanii kuongeza bidii na kufanya kazi kwa bidii lakini isifikie hatua ya mpaka mnatukanana sio vizuri na haipendezi kabisa,” alisema Bella. “Kutukanana ni kitu kibaya sana, tupendane na kila mtu afanye kazi yake. Team pia kila mtu anaweza akawa na team yake lakini team pia zinakuza maugomvi au kutukanana,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents