Burudani

Beka (Natumaini) azungumzia wimbo wake mpya ‘It’s Possible’ na album yake

Msanii aliyewahi kuhit na wimbo wake ‘Natumaini;, Beka Ibrozama anatarajia kuachia wimbo wake mpya ‘It’s Possible’ ambao amedai kuwa ni ujio wake wa tofauti sana.

beka

Beka amesema amejaribu kubadilika na kutoa muziki wa kuchezeka ili kutoa fursa kwa mashabiki wake ili kuwapa muziki tofauti.

“Kuna ngoma yangu mpya inakuja inatwa ‘It’s Possible’ hii ngoma ni tofauti sana kwa sababu watu walimzoea Beka anatoa ngoma za taratibu ila sasa nakuja full kucheza, ni ngoma ambayo watu watacheza, hii ndiyo itakuwa ngoma ya kwanza kwa Beka ya kuchezesha,” ameiambia Bongo5.

Pia Beka amezungumzia ujio wa album yake mpya itakayokamilika mwakani.

“Project ya Band ipo sana, na mimi namalizia nyimbo za album ya bendi nikishamaliza ngoma za album ya bendi nitakuwa rasmi tuanza kuitangaza band, hii album nikimaliza ndo nina mipango ya bendi itakuwa wazi, kwa sababu siwezi kuanzisha bendi wakati sina album. Kwahiyo album yangu itakuwa na nyimbo nane au kumi. Nina imani itauza tu. Ukiona msanii hawezi kuuza album ujue huyo hajui, lakini mimi kwa album na nyimbo nilizozitengeneza lazima utanunua kutokana na kitu nilichokiimba ndani, lakini wasanii wa bongo hawawezi kutoa album kutokana na nyimbo zao hawaziamini.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents