Technology

Beats Music kuwekwa kwenye Iphone na Ipad zote kuanzia mwakani

Kampuni ya Apple imedai kuwa app ya Beats Music itakuwa sehemu ya software ya iOS kuanzia mapema mwakani na itapatikana kwenye iPhone na iPad zote.

beats-music-hero

Financial Times limedai kuwa Beats itakuwa sehemu ya iOS mapema March ikiwa ni jitihada za Apple kuwafanya watumiaji wa iTunes kuijaribu huduma hiyo ya kustream nyimbo watakaoweza pia kulipa kupitia huduma ya Apple Pay kwaajili ya malipo ya kila mwezi ya huduma hiyo.

Apple iliwalipa dola bilioni 3 kampuni baba ya Beats Music, Beats Electronics ya Dr Dre mapema mwaka huu. Beats Music inatarajiwa kuwa mshindani mkuu wa huduma zingine za aina hiyo hasa Spotify na Rhapsody.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents