Burudani

BBA Hotshots: Washiriki wa Kenya, Uganda, na Nigeria watolewa mchezoni, Laveda aponea chupuchupu

Mtanzania Laveda Jumapili October 19 aliponea chupuchupu kwa kubaki kwenye jumba la Big Brother Africa, huku akiwashuhudia washiriki wenzake watatu wa kike wakitoka mchezoni.

esther-lillian-sabina
Sabina, Lilian, Esther

Esther (Uganda) , Lilian (Nigeria) pamoja na Sabina (Kenya) ndio washiriki walioondolewa katika shindano hilo usiku wa jana ikiwa ni ‘eviction’ ya pili toka shindano lianze.

Hadi sasa washiriki watano wa kike wametoka katika shindano hilo na kufanya idadi ya washiriki wa jinsia ya kike kubaki 8 huku wanaume wakiwa 13.

Nchi za Zambia, Mozambique, Kenya, Uganda and Nigeria kila moja imeshapoteza muwakilishi mmoja hivyo zote zimebaki na muwakilishi mmoja mmoja tu mjengoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents