Burudani

BASATA lina siku 7 tu kubaini ukweli kuhusu skendo ya Sitti Mtemvu

Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limeanza kuifanyia uchunguzi skendo inayomkabili Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu kuhusiana na kudanganya umri wake. Baraza hilo lina siku saba tu kukamilisha kazi hiyo.

IMG_5055

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni, Juma Mkamia aliiambia gazeti la Champion kuwa serikali imelikabidhi suala hilo kwa Baraza la Sanaa la Taifa ili wafanye uchunguzi.

“Tayari tumeshalikabidhi kwa Basata na tumewapa muda wa wiki moja kisha watatupa majibu na ushauri juu ya walichokigundua , baada ya hapo sisi tutajua nini kifanyike na kutoa tamko rasmi,” alisema Mkamia.

Nyaraka ambazo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha Sitti alizaliwa Mei 31, 1989 na si Mei 31, 1991 kama inavyoeleza kamati ya Miss Tanzania iliyo chini ya mratibu wa shindano hilo , Hashim Lundenga.

Baadhi ya nyaraka hizo ni paspoti inayodaiwa ni ya Sitti iliyolewa Frebuari 15 ,2007 ikionyesha amezaliwa 1989, Pia leseni ya udereva aliyoipata huku Texas, Marekani inaonyesha mrembo huyo amezaliwa Mei 1989.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents