Burudani

BASATA kumvua Sitti Mtevu Umiss Tanzania ikibainika alidanganya umri

Sakata la umri la Miss Tanzania 2014 Sitti Mtevu limeendelea kuchukua sura mpya baada ya Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kudai kuwa litamvua taji hilo endapo watagungua kasoro za umri zinazodaiwa.

IMG_5058

Akizungumza na gazeti la Nipashe, Katibu Mkuu wa Basata, Geoffrey Mwingereza , alisema wanasubiri uchunguzi wao ukamilike na wakibaini kuwepo kwa udanganyifu watamvua taji hilo. Wakati Mwingereza akielezea taarifa hiyo, viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wanatarajia kukutana leo jijini Dar es salaam kwajili ya kujadili sakata hilo.

Akizungumza na gazeti hilo jana, Naibu Waziri wa Wizara ya Michezo, Juma Mkamia alisema serikali imelisikia sakata la mrembo huyo na wamamua kuitisha kikao ili kulifanyia kazi. “Siwezi kukuambia hatua gani zitachuliwa, ila kesho, (leo) tutakuwa na kikao , serikali haiwezi kukaa kimya , kuna vyombo vyake vinalifanyia kazi,” alisema Mkamia.

Aliongeza kuwa yeye alikuwa nje ya Dar es Salaam lakini kuna maelezo aliyoyatoa na yameanza kufanyiwa kazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents