Burudani

BASATA: Diamond amestahili kukabidhiwa bendera ya Taifa kwajili ya show yake ya ufunguzi wa AFCON 2017 (Audio)

Kumekuwa na sitofamu katika mitandao ya kijamii kuhusu ni nani anastahili kukabidhiwa bendera ya Taifa ili kuwakilisha nchi, baada ya Diamond Platnumz kukabidhiwa bendera ya Taifa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye kwajili ya show yake ya kutumbuiza ufunguzi wa michuano ya Afcon 2017 inayofanyikia nchini Gabon weekend hii.

Diamond akikabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye

Mashabiki wengi katika mitandao hiyo wamekuwa wakizozana bila kupata jibu kwamba ni kwanini Diamond alikabidhiwa bendera hiyo kwa ajili ya kuwakilisha Tanzania wakati anaenda kufanya show yake binafsi.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii kuhusu suala hilo Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza amesema bendera ya Taifa anaweza kupewa mtu yeyote ambaye anaenda nje ya nchi, na safari yake ina manufaa kwa taifa lake.

“Suala wa Waziri Nape ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ndani ya Wazira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumkabidhi Diamond bendera ya Taifa ni jambo zuri kwa sababu ingawa Diamond anakwenda kufanya show yake lakini tukumbuke yule ni mtanzania pekee pale ambaye anakwenda kuliwakilisha Taifa lake kwa show yake mbele ya maelfu ya watu Afrika nzima, jina lake linatambulika pale lakini wao wanamtambua yule kama mtanzania na hata akifanya vizuri sifa zinaenda kwa yeye pamoja na Taifa lake,” alisema Nngereza.

Pia Nngereza alidai mtanzania yeyote anaweza kukabidhiwa bendera ya katifa kama anaenda kufanya tukio lolote ambalo linaweza kuipatia sifa nchi yake kwa namna yoyote.

“Mtu yoyote ambaye anaenda nje ya nchi kwa ajili ya matamasha makubwa au kama kuna namna ambavyo anaenda kufanya kitu ambacho kimpatia yeye faida pamoja na Taifa lake anaweza kukabidhiwa bendera, awe mtanzania tu. Kwa hiyo hata ukiwa mtangazaji, mchezaji, vikundi vya ngoma na sanaa mbalimbali wanaweza kukabidhiwa bendera kama wakihiitaji kwa sababu kuna wengine hawatoi taarifa kuhusu matukio yao lakini kama ukitoa taarifa na mamlaka ikaona kuna umuhimu wa kufanya tunafanya hivyo kwa sababu ni kwa ajili ya taifa letu,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents