Burudani

Barnaba kumfuata Fally Ipupa Ufaransa kumalizia collabo yao

Barnaba anatarajia kwenda nchini Ufaransa ambako atamalizia kurekodi collabo yake na Fally Ipupa.

Barnaba akifanya yake

“Panapo majaliwa katikati ya mwezi ujao naenda Ufaransa. Nikitoka Ufaransa narudi tena New York na baada ya hapo narudi Dar. Kwa ajili ya Hawalade lakini pia kwa ajili ya project nyingine. Kwa sababu mimi pia ni balozi wa malaria no more, kwa hiyo naenda kama balozi ambaye naenda kuchukua elimu kidogo,”. Barnaba aliambia BongoDot Home ya 100.5 Times FM.

“Lakini Ufaransa naenda kwa ajili ya Fally Ipupa. Naenda kufanya collabo nae na wimbo wangu pia nafanya nae. Huo wimbo ulifanyika ulikuwa nusu hakumaliza. Kwa hiyo inabidi nimfate kule tumalizie kule. Masters nitafanyika kule na video ntafanyia kule panapo majaliwa.

Source:Tovuti ya Times FM

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents