Michezo

Barnaba amuomba radhi Ice Boy aliyedai kuchelewesha mafanikio yake

By  | 

Rapper Ice Boy ambaye sasa hivi anafanya vizuri na wimbo ‘Binadamu’ hivi karibuni alisema kuwa Barnaba amechelewesha mafanikio yake.


Barnaba Boy akiwa na Ice Boy

Kutokana na kauli hiyo ya Ice Boy, Barnaba amemuomba msamaha.

Akiongea katika kipindi cha E-Newz ya EATV, Barnaba amesema “Naomba tena radhi kwa jamii kwa kauli ya Ice aliyosema kwamba mimi ndiye nimemchelewesha kufanikiwa katika muziki wake kwakuwa sipendi kugombana na kukwanzana na mtu, namuomba radhi kupitia E-Newz kwamba anisamehe kwa makosa yangu.”

Barnaba aliwahi kumtaja Ice Boy kuwa mmoja wa wasanii wa label yake ya High Table Sound. Hata hivyo hitmaker huyo ‘Loverboy alisema siri ya mafanikio si kuvaa vizuri, kula vizuri au kuishi pazuri bali ni kuwa na heshima na kuepukana na malumbano na ugomvi usio wa lazima.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments