Burudani

Barnaba amtolea nje mke wake kutumika kama model kwenye video za wasanii wengine

Muimbaji na mtunzi wa nyimbo, Barnaba Elias amedai kuwa baada ya kumtumia mke wake ‘Mama Steve’ kama model kwenye video ya wimbo wake ‘Wahalade’, ameanza kupata usumbufu mkubwa kutoka kwa wasanii wengine wakimtaka mke wake atokee kwenye video zao, kitu ambacho hawezi kuruhusu.

“Mimi niliamua nimtumie kwa mara moja tu kwa sababu mimi ni wife wangu, sihuruhu mtu yoyote amtumie wala sipendi hata akawa na nini, mimi sitaki,” ameiambia Bongo5. “Mimi nilimtumia kwa sababu niliona anafaa, she is beautiful, nikaona acha ni mtumie kwa mara moja. Siruhusu mtu kufanya hivyo na yeye mwenyewe anajua mimi sipendi mtu afanye hivyo. Watu wapo wanaosumbua na mimi nawaelekeza sitaki mke wangu afanye hivyo na ana biashara zake,” ameongeza Barnaba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents