Burudani

Barnaba alizwa na wezi, aomba walau wamrudishie passport yake

Usiku wa kuamkia leo Barnaba ameibiwa begi lake lililokuwa ndani ya gari lake likiwa na vitu vya thamani ambavyo ni pamoja na baadhi ya kazi zake ambazo hazijatoka zilizokuwa kwenye hard disc, kamera na laptop mbili.

Barnaba amepost ujumbe Instagram kuwaomba wasamaria wema kumrudishia na kutoa maelezo jinsi ya kuwasiliana naye na kati ya vitu vilivyopotea ipo pia hati yake kusafiria(passport).

Ameandika:

“Za asubui Ndugu Zangu wapendwa Usiku wa kuamkia Leo Nimeibiwa Begi langu Dogo Tu si Kubwa Sana ambalo lilikuwa ndani ya Gari langu | lakini ndani Yake Kulikua Na Laptop ???? za mac mbili moja Pro x moja Letina ya ukubwa Kidogo Theni Kuna external mbili moja Rangi Ya orange ???? moja Ya kijani Na Kuna File Zangu zilikua Na Mikataba Mbali Mbali lakini Kikubwa zaidi Ndani Yake Kuna PASPORT Yangu ambayo Ukifungua ndani Inasoma Jina La ELIASI BARNABASI INYASI and Kuna Vitu Vingi Sana Vidogo vidogo Vyenye Thamani Kubwa Kama Camera ????Na vingine Lakini Naomba sana Sana Waungwana Kama Kuna mtu Yotote atabaini au kujua Vilipo au hata kupelekewa Basi Naomba wasamalia Wema mnirudishie Au kuniletea Na Napatikana kwa No 0743505010 Mungu Awabariki Na naamini Aliyenavyo ajaiba Bali amepitiwa katika njia ya kutafuta Ridhiki Nami kwa jina la mungu nitamsamehe Na nimesamehe ila Kama Ana Rohoo nzuri Na ameguswa Basi Naomba waungwana mnipigie hata Kama Umeokota ????????” Alipost Barnaba

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents