Burudani

Barnaba ajifananisha na Messi, asema ni ngumu kubadilisha ‘menejimenti’

Muimbaji na mtunzi mahiri wa nyimbo, Barnaba amesema hana mpango wa kufuata nyayo za wasanii wenzake waliokuwa THT, Amini na Linah waliobadilisha uongozi unaosimimia kazi zao.

Barnaba

Barnaba ambaye wiki hii aliachia wimbo wake mpya akiwa na Vanessa Mdee, amedai hawezi kuondoka kwenye kampuni aliyotoka nayo mbali na kuwekeza fedha nyingi kwenye kazi yake.

Amedai kuwa kama kuna kampuni inayotaka kumchukua basi ijiandae kufanya kama zinavyofanya klabu za soka zinapokuwa zikisajili wachezaji kutoka klabu zingine. “Namna uwekezaji alioufanya mkurugenzi wangu ni mkubwa zaidi kuliko mtu atakayetaka kunichukua,” alikiambia kipindi cha Power Jams cha EA Radio.

“Kama anataka anichukue, aninunue kama Messi, amlipe kocha, amlipe na mchezaji. Kwasababu menejimenti yangu ina uwezo mkubwa kuliko hata hiyo inayotaka kunichukua.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents