Michezo

Barcelona wazidi kutawala ligi ya Hispania

Timu ya Barcelona imezidi kuonyesha ubora wake kwa kucheza mechi 35 kwenye ligi ya Hispania (La liga) bila kufungwa baada ya kushinda kwa magoli matano kwa moja dhidi ya Vallicano.

2792652

2792752

Barcelona jana usiku wakiwa uwanja wa ugenini walicheza na wenyeji wao Rayo Vallecano na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli matano kwa moja.

Katika mchezo huo mchezaji bora wa dunia kwa mara tano Lionel Mess alifanikiwa kufunga magoli matatu (hat trick) na mengine mawili yakifunga na Rakitic na Arda Turan huku goli la kufutia machozi la Vallecano likifungwa na aliyewahi kuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United Manucho.

Mpaka sasa Barcelona wanaongoza ligi hiyo ya Hispania wakiwa na point 69 wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye point 61.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents