Michezo

Barcelona kuamua mkataba mpya wa Messi

Klabu ya Barcelona itaangalia uwezo wao ili kumpatia Lionel Messi mkataba mpya wenye nyongeza ya mshahara itategemea uwezo wao wa kuvutia mapato kutoka kwa wadhamini na uuzaji wa wachezaji ,amesema mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo Oscar Grau.

Mkataba wa Messi unakamilika 2018 na anatarajia kupewa mkataba mpya huku ikiripotiwa huenda akapewa kitita cha paundi milioni 21 wanazopata Luis Suarez na Neymar.

”Tunahitaji wachezaji wazuri lakini pia lazima kuwa na kipaumbele ”,aliongezea.

La Liga huweka mkataba na kila klabu kuhusu matumizi yao kila mwanzo wa msimu, ambapo huyazuia mabodi kutotumia zaidi ya asilimia 70 ya bajeti yake ya mapato.

Mikataba yenye mishahara mikubwa waliopatiwa Suarez na Neymar ambazo zitakamilika 2021, huchukua kiwango kikubwa cha matumizi ya timu hiyo.

Messi ambaye kwasasa ana umri wa miaka 29, anaripotiwa kupokea paundi milioni 19 na Grau anasema kuwa nyongeza yoyote lazima ifikiriwe sana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents