Habari

Baraza la habari laishtaki Tanzania mahakama ya EAC

Baraza la Habari nchini Tanzania limewasilisha kesi mahakamani kupinga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo Novemba mwaka jana.

Nape Nnauye Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika Serikali ya Awamu ya Tano

Baraza hilo limewasilisha kesi hiyo katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) likishirikiana na mashirika mawili ya kutetea haki za kibinadamu; Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania.

Baraza hilo linaaka baadhi ya vifungu vya sheria, ambavyo wanasema vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza vifutwe.

Wanasema vinakiuka matakwa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zinataka nchi wanachama kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba wa kuundwa kwa jumuiya hiyo.

“Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unahimiza umuhimu wa kufuata kanuni za utawala bora, utawala wa kidemokrasia, utawala wa sheria, uwajibikaji, uwazi, haki kwa wote, usawa wa kijinsia na kuheshimu haki za binadamu,” baraza hilo linasema kupitia taarifa iliyotiwa saini na katibu mtendaji Kajudi Mukajanga.

“Tanzania inatakiwa kuchukua hatua za kuhakikisha haki zote zilizotajwa katika mkataba huo zinafuatwa na kutekelezwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents