Habari

Bamboo: Mungu aliniambia ‘sikukuita Bamboo’, aelezea sababu za kubadili jina na kuwa Abraham

Rapper mkongwe wa Kenya Simon Kimani a.k.a Bamboo ambaye kwa sasa ameokoka, hivi karibuni ametangaza kubadili jina lake kutoka Bamboo ambalo amekuwa akilitumia katika muziki wa kidunia na sasa anataka aitwe Abraham (Ibrahim).

Bamboo22

Rapper huyo tayari amebadili jina lake katika akaunti yake ya facebook na kuwa Abraham Bamboo, na kuelezea sababu za yeye kubadili jina:

“Mungu aliniambia kitu, alisema ‘sikukuita “Bamboo” dunia ndiyo ilikuita hivyo lakini mimi nilikuita kama nilivyokuumba na jina lako ni “Abraham”. Abraham Bamboo linaweza kuwa jina lako kisanii . “ aliandika Bamboo katika akaunti yake ya Facebook.

bamboo

Abraham Bamboo ni kaka wa mastaa wengine wa Kenya Victoria Kimani pamoja na ambao wote ni wasanii wa muziki

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents