Michezo

Balotelli: Tukiwashinda Costa Rica nataka malkia wa Uingereza anipige busu!!

Matumaini ya England kufuzu raundi ya pili ya kombe la duniani ni ya kupumulia kwa mashine baada ya jana kufungwa 2-1 na Uruguay.

article-2663051-1EF09EE300000578-771_634x418
Balotelli anadai Italia ikiwashinda Costa Rica apigwe busu la shavuni na malkia wa UK

Kocha Roy Hodgson anasali ili Italia iwashinde Costa Rica leo ili England ibaki kwenye michuano hiyo ya kombe la dunia. Kutokana na hilo, Mario Balotelli amedai kuwa kama akisaidia Italia ishinde basi apewe busu kutoka kwa Malkia wa Uingereza.

article-2663051-1EEDA8D600000578-259_634x421

Mshambuliaji huyo alitweet: ‘If we beat Costa Rica I want a kiss, obviously on the cheek, from the UK Queen. (‘Tukiwashinda Costa Rica nataka busu, ni wazi kwenye shavu kutoka kwa malkia wa Uingereza)

Balotelli alifunga goli la ushindi wakati Italia ilipokutana na England wiki iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents