Michezo

Bale ajifunga ndani ya Madrid mpaka mwaka 2021

Galeth Bale ameongeza mkataba wa miaka mitano wa kuichezea klabu ya Real Madrid, mpaka mwaka 2021 kwa mujibu wa gazeti la Marca la nchini Hispania.

Bale

Mkataba huo utamfanya mchezaji huyo kuwa mchezaji wa pili wa Madrid kulipwa mshahara mkubwa wa Euro milioni 10 kwa mwaka akiwa analipwa sawa na nahodha wa timu hiyo Sergio Ramos huku wakiongozwa na Cristiano Ronaldo ambaye mkataba wake mpya haujawekwa wazi kiasi anacholipwa kwa sasa.

Bale alifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri kwenye michuano ya Euro iliyomalizika mwazi Julai mwaka huu huko nchini Ufaransa kwa kuisaidia timu yake ya taifa ya Wales kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Mwanzoni klabu ya Manchester United ilionekana kutamani kumsajili mchezaji huyo kabla ya kuvunja tetesi hizo kwa kumsajili Paul Pogba kwa usajili wa paundi milioni 89 ulioweka rekodi ya dunia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents