Habari
Bajeti ya dola bilioni 19 ya safari ya Mars yaidhinishwa na baraza la senate Marekani
Safari ya Marekani kwenda katika sayari ya Mars imekwiva.
Kwa mara ya kwanza katika historia, baraza la senate la nchi hiyo limeidhinisha bajeti ya dola bilioni 19.5 kuwezesha safari hiyo itakayoratibiwa na NASA.
Senate linaitaka NASA kuhakikisha kuwa inapeleka watu kwenye sayari hiyo nyekundu katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Ndoto za NASA kwenda Mars zimekuwepo tangu ianzishe satellite inayozunguka kwenye ‘orbit’’ yake miaka 45 iliyopita.