Burudani

Babu Tale awashauri wasanii kutoa album na kuacha kuhofia kuibiwa

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amewataka wasanii wa Tanzania kuacha kuogopa kutoa album kwa madai ya kuogopa kuibiwa.

Babu Tale akiwasili jijini Mwanza

Akizungumza na Planet Bongo ya East Africa Radio, Tale alisema zipo nchi ambazo zinaongoza kwa wizi wa kazi za wasanii lakini bado wasanii wao wanatoa album.

“Wizi upo dunia nzima,” alisema Tale. “Ukienda Nigeria kuanzia airport wanafanya piracy. Hata Marekani, nafikiri ndio nchi ambayo inatushinda sisi hata kwa mambo ya digital lakini still bado wanatoa album na wanauza,” alisisitiza.

“Album ni heshima ya msanii, yaani kama hauna album you are nothing! Heshima ya msanii ni album, mauzo yapo kama unauza kwenye mitandano milioni moja jiulize ni watanzania wangapi hawatumii internet na wanahitaji kupata kazi?

Babu Tale ameimba nyimbo imetoka jana wanaipataje? Sisi ndio tunawapa ajira hawa pirates, hakuna nchi inaongoza kwa piracy kama India, lakini wanatoa album na wanatoa filamu zao! Biashara inatakiwa imani, ukianza kuogopa nitaibiwa, huwezi pata hela.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents