Burudani

Baba yake Beyonce adai kuwa mwanae na Jay Z walisambaza tetesi za talaka kukuza mauzo ya tiketi ya ziara yao

Baba yake na Beyoncé anadai kuwa mwanae na Jay Z walisambaza kwa makusudi tetesi za talaka kukuza mauzo ya tiketi za ziara yao ya ‘On The Run’.

article-2736267-20C65AEA00000578-692_634x757
Jay Z akimbusu mkewe Beyonce kwenye MTV VMA wakiwa na mtoto wao Blue Ivy

Mathew Knowles alitoa kauli hiyo ya kushtusha alipokuwa akihojiwa katika The Roula And Ryan Show kwenye kituo cha redio cha 104.1 KRBE mapema wiki hii. Mathew amedai kuwa mambo kama hayo hufanyika na huitwa ‘Jedi mind trick’. Kwa mujibu a mtandao wa Radar Online, Mathew alidai kuwa hata yeye ameshafanya hivyo wakati wa ziara.

article-2736267-20DB77F900000578-605_634x917
Mathew akiwa na mwanae Beyonce

Alipoulizwa kama ile clip ya Jay Z na Solange wakigombana kwenye lift kama walitaka pia itoke, Mathew alijibu: ‘All I know is the Jedi mind trick. Everyone’s talking about it. Ticket sales went up. Solange’s album sales went up 200%!’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents