Tragedy

Baba Levo apata ajali akiwa ndani ya basi la AM lililogongana na Coaster

Msanii wa kundi la 2mbili wa Town, Baba Levo amepata ajali baada ya basi la kampuni ya AM Coach alilokuwa amepanda kugongana na Coaster.

Jux na Baba Levo

Kwa mujibu wa Millardayo.com, ajali hiyo imetokea kwenye pori la kijiji cha Uluwila ambapo alikuwa anatokea Tabora kwenda Mpanda. Inadaiwa kuwa dereva wa Coaster alikuwa akikwepa barabara mbovu na hivyo kuhamia upande ambao basi la AM lilikuwa likija na hivyo kugongana uso kwa uso.

Baba Levo amesema ameumia usoni na mwilini kwa kuchanwachanwa na vioo vya mbele vilivyopasuka kwenye basi.

“Ameweza kuona kuna baadhi ya watu wamefariki ambapo kati yao ni waliopasuka vichwa na shingo,” umeandika mtandao huo. Coaster hiyo inadaiwa kufumuka upande wake wa juu huku kukiwa bado na abiria waliobanwa kwenye Coaster hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents